Matthew 1:16-20


16 anaye Yakobo akamzaa Yusufu ambaye alikuwa mumewe Mariamu, mama yake Isa, aitwaye Al-Masihi.
Al-Masihi maana yake ni Masiya , yaani Aliyetiwa mafuta.

17Hivyo, kulikuwepo na jumla ya vizazi kumi na vinne tangu Ibrahimu mpaka Daudi, vizazi kumi na vinne tangu Daudi hadi wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli, na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho kwenda utumwani Babeli hadi Al-Masihi.

Kuzaliwa Kwa Isa Al-Masihi

(Luka 2:1-7)

18 cBasi Kuzaliwa kwake Isa Al-Masihi kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 dKwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, aliazimu kumwacha kwa siri.

20 eLakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.
Copyright information for SwhKC